Habari Za Un

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Ally Mwamzola: Vijana tushiriki kuanzia kuandaa hadi kutekeleza ‘Mkataba wa siku zijazo’

    10/05/2024 Duración: 03min

    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Yeye akiwa anapeperusha bendera ya vijana kwa kuzingatia kuwa pia ni Mratibu wa Mradi wa Ujumbe wa Vijana wa Afrika kwenda Umoja wa Mataifa anayataja mambo matatu ambayo katika mkutano huu vijana walikuwa wanayalenga zaidi. Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.

  • Peter Njenga: Mchezo wa riadha watumika kukaribisha wageni wa mkutano Kenya

    10/05/2024 Duración: 01min

    Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Bwana Njenga akaoanisha michezo na amani.

  • 10 MEI 2024

    10/05/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) unaofunga pazia leo, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa hotuba yake kwa waandishi wa habari, na tutasikia ujumbe wa washiriki wengine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitam

  • Guterres: Afrika inaweza kuwa jabalí la nishati jadidifu

    10/05/2024 Duración: 09min

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Katibu Mkuu Guterres [GUTERESH] amesema dunia inakabiliwa na majanga lukuki, lakini Afrika ndio inaathiriwa vibaya kwa kiasi kikubwa.Bara la Afrika linatikiswa na hali mbayá ya hewa kupindukia, ikichochewa na janga la tabianchi ambalo halijasababishwa na bara hili. Kuanzia mafuriko makubwa mashariki hadi ukame mkali kusini.Afrika inaweza kuwa jabali la nishati jadidifu, amesema Guterres,  kwani ina hifadhi ya asilimia 30 ya madini muhimu kwa ajili ya nishati jadidifu, na asilimia 60 ya rasilimali ya sola au nishati ya jua. Lakini katika miongo ya karibuni, imepokea asilimia mbili tu ya uwekezaji kw

  • Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuinua uchumi na kusongesha agenda ya SDGs - Zahra Salehe

    09/05/2024 Duración: 05min

    Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu. Mfano ni Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ulifanyika hivi karibuni na mmoja wa waliohudhuria ni Zahra Salehe, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, ICCAO Tanzania ambaye katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii tunapata kufahamu baadhi ya malengo yanavyotekelezwa na shirika lake nchini Tanzania. 

  • Jifunze Kiswahili: Tofauti ya “Adili na Idili.”

    09/05/2024 Duración: 52s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”

  • 09 MEI 2024

    09/05/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika kazi za Zahra Salehe na timu yake ya ICCAO nchini Tanzania katika kusongesha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza na asasi za kiraia Nairobi Kenya, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki. Leo mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia umeng’oa nanga mjini Nairobi Kenya ukiwaleta pamoja washiriki takriban 1500 kutoka kila kona ya dunia wakifanya majadiliano ya awali na kutoa takwimu kuelekea mkutano wa wakati ujao utakaofanyika New York Marekani mwezi Sepemba mwaka huu. Umoja wa Mataifa Kenya ndio mwenyeji wa mkutano huo ambapo Mratibu Mkazi wa Umoja huo nchini humo Dkt. Stephen Jackson amesema taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa mstari wa mbele kwenye kusongesha ushirikiano wa kimataifa tangu uhuru wake.Huko Gaza takriban watu 80,000 wamekimbia Rafah tangu Jumatatu wiki hii wakati mashambulizi ya Israel yakishika kasi usiku kucha kuamkia leo ndani na katika viunga vya

  • Hatuna uhakika wa kuitimiza SDG5 kwa 100% lakini tunaweza kufikia hata 90% - Abeida Rashid Abdallah

    08/05/2024 Duración: 03min

    Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 anajibu swali aliloulizwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kwamba Je, Lengo namba 5 la Maendeleo Endelevu linalohamasisha usawa wa kijinsia litafikiwa huko Zanzibar kufikia mwaka 2030?

  • Mafuriko katika Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki yaathiri watu 637,000

    08/05/2024 Duración: 01min

    Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao. Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limetoa takwimu hizo likinukuu ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, huku ikisema kuwa idadi inazidi kuongezeka kila uchao.IOM kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na Nairobi, Kenya inasema mvua hizo za masika zimesababisha mafuriko makubwa, maporomoko ya udongo na kuharibu miundombinu muihmu kama vile barabara, madaraja na mabwawa ya maji.Mkurugenzi wa IOM Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika Rana Jaber anasema mafuriko hayo ya kipekee na yaliyosababisha uharibifu yameibua ukweli mchungu wa mabadiliko ya tabianchi, kwa kusababisha vifo na kufurusha watu makwao, watu ambao sasa

  • 08 MEI 2024

    08/05/2024 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, na wakimbizi wanaorejea nchini Sudan Kusini kutoka Sudan. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni?Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao.Katika makala Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kika

  • Wahamiaji waliorejeshwa Sudan Kusini kutoka Sudan wanasema asante IOM

    08/05/2024 Duración: 01min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao. Waswahili husema “Mkataa kwao mtumwa” na hili ndio hasa alilowaza Bi. Lydia John Wol Mabior ambaye alikuwa ukimbizini nchini Sudan lakini huko nako vita ilipoanza akakumbuka usemi “Nyumbani ni nyumbani hata kama vichakani” kwani ilikuwa si hali. Anasema, “Nilipokuwa Khartoum sikulala usiku wala mchana, niliona ni bora nije kuteseka Sudan Kusini. Na leo nina furaha sana kwasababu nimefika nchini kwangu”Lidya ya familia yake miaka kadhaa iliyopita aliikimbia nchini yake ya Sudan Kusini pale vita vilipozuka. Na shukran ziliendee shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM ambalo limefanikisha kumrejesha nchini mwake.“Niliambiwa kuna shirikia lakutusaidia kufika Sudan Kusini, na tangu tumefika hapa eneo la Renk, tumepewa msaada wa kifedha

  • 07 MEI 2024

    07/05/2024 Duración: 12min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako Umoja wa mataifa uko mstari wa mbele kuwapa msaada wakenya wanaotatizika kutokana na mafuriko. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza, Uhamiaji na misitu. Mashinani inatupeleka nchi Haiti, kulikoni? Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea kusisitiza wito wake wa kusitishwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka wote na kuepusha zahma kubwa ya kibinadamu kwa watu wa Gaza. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani amesema “Tuko katika wakati maamuzi kwa ajili ya watu wa Palestina na Israeli na kwa hatima ya Ukanda mzima.Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limezindua Ripoti ya Dunia ya Uhamiaji 2024, ambayo inaonyesha mabadiliko makubwa katika mifumo ya uhamiaji duniani, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao na pia ongezeko la fedha zinazotumwa kimataifa. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope amezindua rasmi ripoti hiyo nchini Bangladesh, nchi ambayo iko mstari wa m

  • UNHCR inawasaidia wakimbizi dhidi ya mafuriko Afrika Mashariki

    06/05/2024 Duración: 03min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linapambana kuhakikisha linawasaidia wakimbizi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Afrika Mashariki dhidi ya madhila yanayosababishwa na mafuriko makubwa kutoka na mvua za El Niño zinazoendelea. Makala hii ambayo video zake zimekusanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR inaanzia Bujumbura Burundi kisha inakupeleka Kenya katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kama inavyosimuliwa na Evarist Mapesa.

  • UNICEF: Watoto walioko Rafah wasihamishwe kwani tayari wako taabani

    06/05/2024 Duración: 01min

    Janga la kibinadamu likizidi kushamiri kila uchao huko Ukanda wa Gaza, shirika la  Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kuwa kuzingirwa kijeshi kwa eneo hilo sambamba na operesheni za ardhini za kijeshi huko Rafah kutasababisha janga kubwa kwa watoto 600,000 waliosaka hifadhi kwenye eneo hilo. Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini New York, Marekani inakumbusha kuwa amri ya kuhamia Rafah, kusini mwa Gaza iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka jana na Israel imefanya eneo hilo sasa kuhifadhi watu wapatao milioi 1.2, nusu yao wakiwa ni watoto wakiishi kwenye mahema au nyumba zisizo kamilifu.Kwa kuzingatia mlundikano wa watoto, wakiwemo wengi walio hatarini wakihaha kuishi, pamoja na ukubwa wa ghasia zinazoendelea na njia za kutumia kukimbia zikiwa na vilipuzi au hakuna njia kabisa , UNICEF inaonya madhila zaidi kwa watoto na operesheni za kijeshi vitaongeza vifo zaidi vya raia na miundombinu ya huduma za msingi iliyosalia kusambaratishwa.Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell amese

  • 06 MEI 2024

    06/05/2024 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama huko Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza, na mafuriko nchini Kenya huku mashirika wakihaha kusaidia waathirika. Makala tunasalia na mada hiyo ya mafuriko Afrika mashariki na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni? Janga la kibinadamu likizidi kushamiri kila uchao huko Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kuwa kuzingirwa kijeshi kwa eneo hilo sambamba na operesheni za ardhini za kijeshi huko Rafah kutasababisha janga kubwa kwa watoto 600,000 waliosaka hifadhi kwenye eneo hilo..Wingu kubwa la mvua likiwa limetanda kwenye mji wa Garsen, ulioko kaunti ya Mto Tana nchini Kenya, Eva Ghamaharo, mama wa watoto watatu anarejea nyumbani akitembea na watoto wake wawili mapacha wenye umri wa miaka mitatu baada ya kununua matumizi ya nyumbani kutoka kioski cha jirani. Watoto hawa wawili mapacha wa kike ni Grace na Jane na wanaonekana na furaha kwani angalau leo mama yao ameweza kuwanunulia kila mmoja pakiti ya maziwa na wa

  • Mafuriko Kenya: UNICEF yapatia wakazi wa Kaunti ya Mto Tana fedha za kujikimu

    06/05/2024 Duración: 02min

    Mvua za El-nino zikiendelea kutikisa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo taifa la Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza limepatia msaada wa hali na mali wakazi wa kaunti ya mto Tana walioathiriwa na mafuriko hayo.  Cecily Kariuki na taarifa zaidi.Video ya UNICEF Kenya inaanza ikimuonesha mkazi huyu wa hapa mji wa Garseni katika kaunti ya mto Tana akiwa amebeba kikapu huku akiwa na watoto wake wawili wakirejea nyumbani.Huyu si mwingine bali Eva Ghahamaro akisimulia yaliyowasibu na msaada ulivyowafikia. Anasema, “Maisha yalikuwa magumu kwa sababu mafuriko yaliharibu nyumba na mashamba. Vyakula vilisombwa. Watu wengi waliteseka sana. Maafisa wa kaunti waliona tunateseka, walitembea nyumba kwa nyumba wakisajili majina watu wenye watoto na wajauzito. Nilikuwa nikipata shilingi 2,750.”Shilingi 2750 ni sawa na dola 20 za kimarekani, na wanapatiwa kila mwezi. Rachael Wamoto ni afisa kutoka UNICEF Kenya na anafafanua kuhusu usaidizi huo amb

  • Wanahabari waweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira

    03/05/2024 Duración: 03min

    Leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira. 

  • Umoja wa Mataifa umeanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko

    03/05/2024 Duración: 02min

    Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Matal Amin iliyoko Baidoa nchini Somalia zaidi ya wananchi 1500 wanahaha huku na kule kurekebisha maturubai yao ambayo hasa ndio makazi yao ikiwa ni maandalizi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kuanza muda wowote. Hali ni hivyo hivyo pia katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rama cade kama anavyotueleza Kiongozi wa kambi hiyo Abdulkadir Adinur Aden anasema “Tunajiandaa na msimu wa mvua ili kupunguza athari za mafuriko, tunatumia maturubai ya plastiki kufunika makazi yetu na pia tunatumia viroba vilivyojazwa michanga ili kuzuia mnomonyoko mafuriko yatakapo tukumba.”Wada

  • 03 MEI 2024

    03/05/2024 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira. Pia tunakupeleka nchini Somalia na Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo, kulikoni? Hii leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na shirikisho la waandishi wa habari duniani, IFJ wametoa ripoti yao ikionesha kuwa ni katika kipindi cha miaka 15 iliyopita waandishi wa habari 44 waliuawa wakiwa wanachunguza masuala ya mazingira. Kampeni ya siku hii ni kwamba kila habari kuhusu mazingira lazima isimuliwe hivyo waandishi wa habari walindwe.Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 kati

  • UNESCO: Waandishi wa habari 44 waliuawa wakichunguza masuala ya mazingira

    03/05/2024 Duración: 02min

    Hii leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na shirikisho la waandishi wa habari duniani, IFJ wametoa ripoti yao ikionesha kuwa ni katika kipindi cha miaka 15 iliyopita waandishi wa habari 44 waliuawa wakiwa wanachunguza masuala ya mazingira. Kampeni ya siku hii ni kwamba kila habari kuhusu mazingira lazima isimuliwe hivyo waandishi wa habari walindwe.Masuala hayo ni pamoja na jinsi sekta ya madini inavyochafua mazingira, migogoro ya ardhi hasa kwenye maeneo yenye maliasili na bila kusahau ukimbizi utokanao na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Kipindi hicho cha miaka 15 ni kuanzia mwaka 2009 hadi 2023.Guilherme Canela, Mkuu wa Kitengo cha Uhuru wa Vyombo vya Habari na Usalama wa Waandishi wa Habari, UNESCO akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesema, tumebaini kuwa waandishi wa habari 44 waliuawa katika kipindi c

página 1 de 5